Home / Masomo ya Biblia / Ushuhuda

Ushuhuda

Tukilijua neno la Mungu hatutaweza kukosa kulishuhudia kwa watu wengine. Imeandikwa 2Wafalme 7:9 "Ndipo wakaambiana mambo haya tuyafanyayo si mema leo ni siku ya habari njema na sisi tunanyamaza mkingoja hata kutakapo pambazuka madhara yatakupata twende tukaambie watu wa nyumba ya mfalme."

Amri ya Yesu yatuwesha kutoa ushuhuda wake. Imeandikwa, Mathayo 28:18-20 "Yesu kwao akasema nao, akawaambia nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niyowaamuru ninyi; na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari."

Sisi wakristo twaweza kuwa hatuna ushuhuda wa macho lakini twaweza kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo. Imeandikwa, Matendo ya mitume 1:8 "Lakini mtapokea nguvu akisha kuwajia juu yenu Roho mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi na Uyahudi wote na Samaria, na hata mwisho wa nchi."