Dhiki

Tunapokua na msongo, maombi yatoa msongo. Imeandikwa, Zaburi 62:1-2 "Nafsi yangu ya mngoja Mungu peke yake kwa kuwa wokovu wangu hutoka kwake yeye ndiye mwamba wangu na wokovu wangu. Ngome yangu, sitatikisika sana."

Dhiki ya ambayo hatuwezi kuepuka yaweza kutusaidia kukua kiroho. Imeandikwa, Warumi 5:3-4 "Wala si hivyo tu ila namfurahi katika dhiki pia; mkijua yakuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi na kazi ya saburi ni udhabiti wa moyo na kazi ya udhabiti wa moyo ni tumaini."

Dhiki nje isiwe dhiki ndani. Imeandikwa, Wafilipi 4:6-7 "Msijisumbue kwa neno lo lote Bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Yesu Kristo."

Katika dhiki twaweza kuwa na amani tukiweka fikara zetu katika Yesu. Imeamdikwa, Isaya 26:3 "Utamlinda yeye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu kwa kuwa anakutumaini."