Dhulumu

Tunashauriwa vipi kuhusu unyanyasaji kati ya watu? Imeandikwa katika Wakolosai 3:19 "Ninyi waume wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao."

Mungu ana chukia zinaa ya maharimu kama vile baba na binti yake kukutana kimwili. Imeandikwa katika Mambo ya Walawi 18:6 "Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu wake mimi ndimi Bwana."

Ujeuri ni dalili ya kutokuwa na uaminifu. Imeandikwa katika Mithali 13:2 "Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri."

Mtu jeuri sio wakutamanika. Imeandikwa katika Mithali 3:31 "Usimhusudu mtu mwenye jeuri, wala usiichague mojawapo ya njia zake."

Mithali 13:3 imeandikwa "Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu."

Faraja kwa anayedhalilishwa, imo katika Biblia; Zaburi 91:1-16 "Aketiye mahali pa siri pake aliye juu atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. Nitasema, BWANA ndiwe kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. Maana yeye atakuokoa na mtengo wa mwindaji, na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya yake atakufunika, chini ya mbawa zake utapata kimbilio; uaminifu wake ni ngao na kigao. Hutaogopa hofu ya usiku, wala mshale urukao mshana, Wala tauni ipitayo gizani, wala uwele uharibuo adhuhuri, ingawa watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe. Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki. Kwa kuwa wewe BWANA ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haita karibia hema yako. Kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote. Mikononi mwao watakuchukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Utawakanyanga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu. Kwa kuwa amekaza kunipenda nitamuokoa na kumuweka palipo juu, Kwa kuwa amelijua jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, nitamuokoa nakumtukuza; kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu."

Mungu ana wapenda wanaonyanyaswa. Imeandikwa katika Warumi 5:5 "Na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho mtakatifu tuliyepewa sisi."

Wanyanyasaji watapata malipo yao. Imeandikwa katika Zaburi 60:11-12 "Utuletee msaada juu ya mtesi, maana wokovu wa binaadamu haufai. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, maana yeye atawakanyaga watesi wetu."

Tumeahidiwa usalama na usingizi usio na hofu. Imeandikwa Mithali 3:21-24 "Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, shika hekima kamili na busara. Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, na neema shingoni mwako. Ndipo utakapokwenda katika njia salama wala mguu wako hautakwaa. Ulalapo hautaona hofu; naam utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. usiogope hofu ya ghafula, wala uharibifu wa waovu utakapofika kwa kuwa bwana atakuwa tumaini lako, naye ata kulinda mguu wako usinaswe."