Sabato

Sabto ilitegenezwa na nani na kwa nani. Imeandikwa, Mwanazo 2:1-2 "Basi bingu na nchi zikamalizika na jeshi lake lote na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanyaakastarehe siku ya saba akaaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya."

Kwanini tuiweke sabato takatifu?. Imeandikwa, Kutoka 20:11 "Maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa."

Kristo alisema sabato ilitegenezwa kwa ajili ya nani?. Imeandikwa, Marko 2:27 "Akawaambia sabato ilifanyika kwa ajili ya wanadamu, si wanadamu kwa ajili ya sabato."

Amri ya nne yasema nini kuhusu sabato?. Imeandikwa, Kutoka 20:8-10 "Ikumbuke siku ya sabato uitakase siku sita ufanye kazi yako yote lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote wewe, wala mwana wako wala binti yako wala mtumwa wako wala mjakazi wako, wal mnyama wako wakufuga wala mgeni aliye ndani ya alango yako. Maan kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo akastarehe siku ya sababa; kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya sabato akaitakasa.."

Mungu ametega nini kati yake na watu wake. Imeandikwa, Ezekieli 20:20 "Zitakaseni sabato zangu zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi mpate kujua mimi ndimi Bwana Munug wenu."

Sabato ni ishara ya utakaso. Imeandikwa, Ezekieli 20:12 "Tena naliwapa sabato iwe ishara kati yangu na wao wapate kujua mimi Bwana, atakasaye."

Katika nchi pya na mbingu mpya watu wa Mungu watamwabudu Mungu vipi?. Imeandikwa, Isaya 66:22-23 "Kama vile mbingu mpya na nchi mpya nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya na sabato hata sabato wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu asema Bwana."

Je Kristo alipokuwa katika dunia hii aliitii sabato?. Imeandikwa, Luka 4:16 "Akaenda Nazareti hapo alipolelewa na siku ya sabto akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake akasimama iliasome."

Je! Siku ya kwanza ya juma nini kilitendeka. Imeandikwa, Mathayo 28:1 "Hata sabato ilipokwisha, ikabambazuka siku ya kwanza ya juma Mariamu magdalina na jule maria wapili walikwenda kulitazama kaburi."

Baada ya kububiwa kwake Jesu wale wanawake walipumzika siku ipi? Imeandikwa, Luka 23:56 "Wakarudi wakafanye manukato na marhamu. na siku yasabato wakastarehe kama ilivyoamriwa."

Je! Ni siku ipi iliyo ya sabato? Kulingana na sheria. Imeandikwa, Kutoka 20:10 "Lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako."

Je! desturi ya Paulo ilikuwa gani kuhusu sabato?. Imeandikwa, Matendo ya mitume 17:2 "Na paulo kama ilivyokuwa desturi yake akaingia mle walimo akahojiana na wao kwa maneno ya maandiko kwa sabatu tatu."

Je Mungu alisema nini kuhusu sheria za Mungu?. Imeandikwa, Mathayo 5:17-19 "Msidhani yakuwa nalikuja kuitangua sheria au manabii la, sikuja kuitangua bali kuitimiliza kwa maana amini nawaabia mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi oja wal anukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie basimtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni bali mtu atakaye zitenda na kuzifundisha huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni."

Je! ni ibada gani ambayo Mungu anaonya isiyo ambatana na amri za Mungu. Imeandikwa, Mathayo 15:9 "Nao waniabudu bure wakifundisha maagizo yaliyo maagizo ya wanadamu.."

Je! Watu wa Mungu watatambikana kwa jinsi gani?. Ieandikwa, Ufunuo 14:12 "Hapo ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu."