Uumbaji

Biblia yatufundisha nini kuhusu Uumbaji? Imeandikwa katika Mwanzo 1:1 "Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi."

Mungu anajionyesha kupitia kwa Uumbaji. Imeandikwa katika Zaburi 19:1 "Mbingu za hubiri utukufu wa Mungu Na anga yaitangaza kazi ya mikono ya yake."

Maumbile yaonyesha kuwa Mungu yupo na kazi yake. Imeandikwa katika "Warumi 1:20 "Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana yanaonekana na kufahamika kwa kazi yake yani uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru."

Mungu alinena navyo vitu vikaumbika. Imeandikwa katika Zaburi 33:6, 9 "kwa neno la Mungu mbingu zilifanyika na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. Maana yeye alisema na ikawa na yeye aliamuru ikasimama."

Mungu aliumba dunia kwa siku sita. Imeandikwa katika Kutoka 20:11 "Maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya saba akaitakasa."

Kwa njia ya nani Mungu aliziumba mbingu na nchi? Imeandikwa katika Wakolosai 1:16 "Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa vilivyo mbinguni na juu ya nchi vinavyoonekana na visivyoonekana ikiwa ni vitu vya enzi au mamlaka vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake." Yohana 1:3 "Vyote vilifanyika kwa huyo wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika

Mungu alikuwa na nia ngani akiumba dunia? imeandikwa Isaya 45:18 "Bwana mungu aliyeziumba mbunu na nchi asema hivi yeye ni Mungu; ndiye aliyeumba duni na kuifanya; ndiye aliye ifanyaimara hakuiumba iwe ukiwa aliiumba iliikaliwe na watu mimi ni Bwana wala hakuna mwingine."

Mungu aliweza vipi kuihudumia dunia aliyo iumba imeandikwa Mwanzo 2:7, 21, 22 "Bwana mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi akampulizia mapuani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai. Bwana akamletea Adamu usingizi mzito naye akalala, kisha akatwa ubavu wake mmoja akafunika nyama mahali pake na ule ubavu alioutowaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke akamletea kwa Adamu."

Ni kwa mfano upi tuliumbwa imeandikwa Mwanzo 1:27 " Mungu akaumba mtu kwa mfano wake kwa mfano wa mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba."

Binadamu alipewa mamlaka gani? Imeandikwa Mwanzo 1:26 "Mungu akasema natumfanye mtu kwa sura yetu watawale samaki wa baharini na ndege wa angani na wanyama na nchi yote pia na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."

Zaburi 8:3-6 "Nikiziangalia mbingu zako kazi ya vidole vyako mwezi na nyota ulizoziratibisha mtu nikitu gani hataumkumbuke na binadamu hata umwangalie umemfanya mdogo punde kuliko Mungu umemvika tajia ya utukufuu na heshima umemtawaza juu ya kazi ya mikono yako umevitia vitu vyote chini ya miguu yake."