Ajira

Waajiriwa wapaswa kufanya kazi kama mungu ndio mwajiri wao imeandikwa Waefeso 6:7-8 "Kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si wanadamu; mkijua yakuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru."

Wajiri lazima wawe waaminifu imeandikwa Medhali 25:13 "Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao."

Wakristo nivema wajulikane ya kuwa ni watu wenye bidii katika kazi zao. imeandikwa Tito 2:9-10 " Watumwa na watii bwana zao wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu, wasiwe waibaji bali wauwonyeshe uwaminifu mwema wote ili wayapambe mafundisho ya mwokozi wetu mungu katika mambo yote."

Je tunapaswa kuwa na haligani katika kazi? imeandikwa Wakolosai 3:23 " Lo lote mfanyalo lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana wala si kwa wanadamu."

Waajiri msiwafanyishe wajiriwa wenu kazi nyingi bila kuwa lipa malipo yanayo faa. imeandikwa Yakobo 5:4 "Angalieni ujira wa wakulima walio vuna mashamba yenu ninyi mliouzuia kwa hila unapiga kelele na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi."

Mtu asiye fanya kazi ameikata ile imani. imeandikwa 1Timotheo 5:8 "Lakini mtu yeyote asiye watunza walio wake yani wale wanyumbani mwake hasa ameikana imani tena ni mbaya kuliko asiye amini."